top of page

BENDI YA SILK ROAD SYMPHONY inatambua kuwa jukumu lake ni hatua moja mbele katika muziki uliotukuka – ikihamasishwa na Tamasha la Ndege – SILK ROAD yenye mtangamano wa tamaduni mbalimbali, ubora wa hali ya juu pamoja na masuala mengine mbalimbali. 

 

Barabara kama ishara ya kule tuendako – muziki kutoka Mashariki kuelekea Magharibi na watunzi kutoka pande mbalimbali za dunia wakieleza upya kuhusu dhana ya ubora (hariri) kulingana na namna  matamasha yanavyoendeshwa katika Karne ya 21. 

 

Wanamuziki kutoka pande mbalimbali za dunia wenye asili tofautitofauti kuanzia New York, Jakarta, Cape Town, Athens, Istanbul, Teheran, Kairo, Dushanbe, Oxford, Rio, Moscow, Beijing, Tokio hadi Berlin.

 

Inaunganisha upekee wa fikra mbalimbali za mtu mmoja mmoja kuhusu ubora na mazingira ya Tamasha la Ndege (SRCB) katika kutoa  maana ya Utamaduni na Muziki ikilinganisha Mashariki na Magharibi, Kaskazini na Kusini – baina ya utunzi - ubora na ala za muziki.

​

BENDI YA SILK ROAD SYMPHONY tunajitambua kama chanzo cha Tamasha la Ndege katika UKANDA WA KIUTAMADUNI WA SILK ROAD. Jukumu letu ni kulinda vyanzo mbalimbali na tofautofauti vinayohamasisha  wapenzi wa muziki duniani kote kwa kutumia njia ya utaalamu wetu na kuimarisha vyanzo mbalimbali vya muziki kwa kuvipatia  msaada madhubuti, halisi, na bayana. 

   

Kwa kiasi fulani, Bendi ya Silk Road Symphony inaona  dhamira yake kama ugunduzi wenye kushirikisha tamaduni mbalimbali kwa nia ya kufanikisha lengo la 18 la Malengo Endelevu ya Utamaduni ambalo bado linakosekana.  

bottom of page