top of page

Usuli

Ukanda wa Kitamaduni wa Silk Road, kama wazo  la zama zetu umekuwa ni fursa ya pamoja kwetu tangu ulipozinduliwa rasmi mwezi Februari, mwaka 2016.

​

Shukrani ziliendee Shirika la Callias kwa kutupatia fursa kubwa ya kusaidia idadi inayoongezeka ya vyanzo vya hamasa katika Ukanda wa Kiutamaduni wa Silk Road. Tunajisikia kuhamasika kwa kuwa kwetu sehemu ya juhudi hizi za kilimwengu na kuwashirikisha watu ambao muziki uliotukuka ni sehemu muhimu ya maisha yao, kutafakari upya wazo la sababu ya kuibuka kwetu kama bendi ya Silk Road Symphony kwa kushirikiana mawazo yao binafsi kuhusu ubora katika Ukanda wa Kitamaduni wa Silk Road

​

Kinachotusukuma sisi kama bendi ni: Tunataka kukufahamu wewe, hadhira yetu ya kimataifa, na kisha tunataka kukualika uwe mtunzi hai na unayejitambua si tu katika Ukanda wa Kiutamaduni wa Silk Road ambao tunauamini sisi bali pia katika  matamasha yetu katika Silk Road Mpya na kwingineko.

​

Sisi kama wasanii, tunaamini kwamba Ukanda wa Kiutamaduni wa Silk Road unatupatia jukwaa la pamoja la hamasa la kubadilishana kile ambacho kila mmoja anakiamini katika Ubora wa muziki: ubora wa msingi wa kibinadamu, kama unavyoelezwa kwa njia mbalimbali za muziki uliotukuka na la kutuwezesha tuunde pamoja nawe mazingira yanayohitajika katika kupata muziki wa kiwango cha ubora wa hali ya juu kabisa.

​

Tunataka kujifunza, kutoka kwako, kutoka ktika Tamasha la Ndege, wewe nini maana ya obora katika muziki kwa kusikiliza pamoja wimbo mmoja kutoka katika orodha yako ya nyimbo ikiwa ni kwa njia ya mtandao, video, au mp3 na kuuacha katika Ukanda kwa ajili ya kusikilizwa na watu wengine.

​

Mwaka 2016 / 2017, tutachangua kutoka katika orodha ya nyimbo za matamasha yetu, kazi moja ya muziki (Utunzi/Ubora/vyombo) katika kazi  zilizotumzwa Ukanda wa Kiutamaduni wa Silk Road na kuijumuisha katika programu yetu.

​

Kama tuzo yako ya kuwa chanzo cha hamasa, Shirika la Callias, litakualika uhudhurie moja ya matamasha yetu katika 'Ukanda wa Kitamaduni wa Silk Road mwaka 2017 / 2018, ambapo utatajwa kama “chanzo cha hamasa” (jina/shirika) katika programu yetu, katika tovuti yetu, na katika taarifa yetu kwa vyombo vya habari.

 

Kwa njia hiyo, utaweza kusaida Bendi ya Silk Road Symphony Okestra katika lengo lake la kutengeneza, kwa njia ya kushirikisha hadhira ya jukwaani na  ya mtandaoni ndani ya Silk Road ya karne ya 21, aina ya majadiliano ya moja kwa moja kwa manufaa yako binafsi, hadhira, Bendi ya SRS, na ubora wenyewe wa utengenezaji muziki.

​

Shukrani za dhati ziwaendee watunzi-washiriki katika Bendi ya SRCB kote ulimwenguni kuanzia New York, Kinshasa, Berlin, Beijing, Paris, Amsterdam,n.k  kwa michango yenu mikubwa!

​

Chanzo cha kwanza cha hamasa kwa tamasha letu la kwanza jijini Berlin ni Walter Hu kutoka Beijing, ambaye alimpendekeza mtunzi wa Kichina, Chen Qigang akiwa na wimbo unaoitwa '5 Elements', ambao tuliujumuisha katika programu yetu, pamoja na wimbo 'Don Juan' wa Richard Strauss na wimbo 'the Firebird' wa Igor Stravinsky. 

 

Tarehe 20Januari, mwaka 2017,mpigasolo wa Bendi ya Silk Road Symphyony alicheza nyimbo za Ligeti, Debussy,na Mozart katika Botanical Garden ya jijini Berlin. Mchoraji wa Kiitali, Flavio de Marco alichora picha 8 zilizotokana na vyanzo hivi vya kimuziki vya hamasa vilivyowasilishwa katika Ukanda wa Kiutamaduni wa Silk Road.

​

Kadiri Watu wengi zaidi wanavyochangia wazo lao binafsi la 'Ubora', ndivyo tunavyojiongezea zaidi hamasa ya pamoja.

bottom of page