top of page

Tamasha la Ndege

 

Onesho kutoka katika Tamasha la Ndege katika Uajemi. Hoopoe, kati kulia, huelekeza ndege wengine kupita kwenye njia ya Sufi.

Tamasha la Ndege au Hotuba ya Ndege (Kiajemi: منطقالطیر‎‎, Manṭiq-uṭ-Ṭayr, pia hujulikana kama مقاماتالطیور Maqāmāt-uṭ-Ṭuyūr; 1177), ni shairi refu la takribani mistari 4500 lililoandikwa kwa Kiajemi na mshairi Farid ud-Din Attar, anayejulikana zaidi kama Uturiwa Nishapur.

 

Katika shairi hilo, ndege wa dunia wanakusanyika ili kumchagua mfalme wao, kwakuwa hawakuwa na mfalme. Hoopoe, ndege mjanja kuliko wote, anapendekeza kuwa  wamtafute Simorgh, ndege wa kufikirika  katika simulizi za  Kiajemi anayefanana kidogo na finiksi wa kimagharibi. Hoopoe anaongoza ndege wenzake,  huku kila ndege akiwakilisha dosari inayosababisha binadamu akose utambuzi. Pale kundi la ndege thelathini wanapofika katika makazi ya Simorgh, kitu pekee wanachokiona ni  ziwa na ndani ya ziwa hilo  wanajiona sura zao wenyewe.

 

Pamoja na kuwa moja ya  mashairi maarufu sana ya Kiajemi, kitabu hiki kinajitegemeza katika sanaa ya matumizi ya neno Simorgh – ndege wa kufikirika katika simulizi za Kiirani ambaye ni ishara inayopatikana mara kwa mara kwenye fasihi ya Sufi, na anayefanana na ndege finiksi – na neno "si morgh" – ikimaanisha kwa Kiajemi"ndege thelathini".

 

Ilikuwa Uchina, usiku mmoja wa manane usio na mbalamwezi,

Simorgh alitokea kwanza katika mwonekano wa kawaida –

Alichanuza mbawa zikaenea angani,

Na minong’ono ya umaarufu wake ikaenea kote;

bottom of page